Jitahidi uwezavyo kuunda nyakati maalum kwa ajili yenu wote wawili. Ingawa huu unaweza kuwa ugonjwa mgumu sana, thamini nyakati za kuwa pamoja ulizo nazo, ambazo usingezipata kama si hivyo.
“Ingawa utunzaji ni mojawapo ya kazi ngumu na zinazohitaji nguvu zaidi tutakazowahi kufanya–na zinahitaji uvumilivu mkubwa na nguvu za kitabia–pia ni jukumu la watu wenye ujasiri na matumaini. Kuwa na nguvu, sherehekea kila ushindi mdogo, cheka inapowezekana na lia inapobidi.” – Tom & Karen Brenner, waandishi wa You Say Goodbye and We Say Hello